• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa makala kuhimiza kuboresha kinga na udhibiti wa maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-29 19:41:11

    Rais Xi Jinping wa China ametoa makala kwenye jarida la Chama cha Kikomunisti cha China CPC Qiushi, ikihimiza kuongeza uwezo wa kusimamia, kukinga na kudhibiti kwa kufuata sheria na kuboresha mfumo wa usimamizi wa afya za umma wa kukabiliana na dharura.

    Makala hiyo imesisitiza kuwa kuhakikisha usalama wa maisha na afya za umma ni jukumu kubwa la usimamizi wa taifa la CPC, na kwamba siku zote inapaswa kuweka kipaumbele usalama wa maisha na afya za umma, na kuhimiza kukinga na kudhibiti maambukizi kwa kufuata sheria.

    Pia imesema, hivi sasa kinga na udhibiti wa maambukizi uko katika kipindi muhimu, kinga na udhibiti wa kufuata utaratibu wa sayansi na sheria ni muhimu sana. Kamati za chama na serikali za ngazi mbalimbali zinatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa pande zote na kufuata sheria, kuendelea kufanya shughuli za kinga na udhibiti kwa wazo la kisheria na njia ya usimamizi wa kisheria, ili kusukuma mbele ujenzi wa uwezo wa usimamizi katika hali ya dharura na kuinua kiwango cha utekelezaji wa sheria na kutawala kwa kufuata sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako