• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China azungumza na wenzake wa Chile na Cuba

    (GMT+08:00) 2020-02-29 19:44:12

    Rais Xi Jinping wa China jana usiku, alizungumzana na rais Miguel Juan Sebastián Piñera Echenique wa Chile kwa njia ya simu.

    Katika mazungumzo yao Rais Xi alisema, maambukizi ya COVID-19 ni tukio kubwa kabisa la afya ya jamii ambayo yameenea kwa kasi na kwa upana, na pia ni vigumu zaidi kudhibitiwa na kukingwa tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Baada ya kutokea kwa maambukizi hayo, China imejipanga kwa pande zote, na wachina wote walishirikiana na kuchukua hatua kali za pande zote katika kudhibiti na kukinga virusi hivyo. Sasa hali ya kudhibiti na kukinga virusi hivyo inaendelea kuboreshwa. Alisema Wachina wana Imani na uwezo kuvishinda vita hivyo.

    Rais Xi Jinping alisisitiza kuwa, katika mapambano dhidi vya virusi hivyo, China inashikilia msimamo wa kujenga mustakabali wa pamoja wa bindamu, na kupeana habari na Shirika la Afya Duniani WHO na jumuiya ya kiamtaifa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuzuia kuenea kwa virusi hivyo duniani. Alishukuru serikali na watu wa nchi mbalimbali ikiwemo Chile kwa kuiunga mkono China kwa njia mbalimbali.

    Kwa upande wake Rais Pinera alitoa salamu za dhati kwa niaba ya serikali ya Chile na watu wake, na kuahidi kuunga mkono wachina katika kupambana na virusi vya COVID-19.

    Aidha rais Xi Jinping pia alizungumzana na rais Miguel Díaz-Canel Bermúdez wa Cuba kwa njia ya simu. Alisema tangu kutokea kwa maambukizi ya COVID-19, rais Diaz-Canel alikwenda ubalozi wa China nchini Cuba na kueleza uungaji mkono wa Cuba kwa China, hii ilionesha urafiki wa jadi kati ya China na Cuba. Cuba ilifuatilia maoni ya kitaalamu ya WHO na kulinda mawasiliano na ushirikiano wa kawaida kati ya nchi hizo mbili, pia iliheshimu na kushirikiana katika kazi za kudhibiti na kukinga za China, hivyo China inapongeza maelewano na uungaji mkono wa Cuba.

    Rais Diaz-Canel alisema Cuba itaendelea kushirikiana na China na kupenda kutoa misaada kadiri iwezekanavyo kwa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako