• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakabiliana na uwezekano wa kuingia kwa COVID-19 kutoka nje

    (GMT+08:00) 2020-03-01 18:29:09

    China imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na uwekezano wa kuingia kwa virusi vipya vya korona COVID-19 kutoka nchi za nje.

    Idara Kuu ya Forodha ya China imesema inafuatilia na kufanya tathmini kwa wakati kuhusu hali ya maambukizi ya COVID-19 ndani na nje ya nchi, na imeanzisha utaratibu wa kuwataka watu wote wanaokuja China watoe ripoti kuhusu afya zao kabla ya kufika, na pia inaangalia kwa hatua kali afya za watu wote wanaokwenda nje ya nchi. China imesisitiza kuwa itarekebisha mipango ya teknolojia ya kukinga na kuzuia maambukizi ya virusi na kutoa taarifa husika na jamii ya kimataifa.

    Wakati huohuo, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema serikali ya China inazingatia sana afya na usalama wa wachina wanaoishi katika nchi zilizoathiriwa vibaya na COVID-19 zikiwemo Korea Kusini, Japan, Italia na Iran na imewataka wafuate hatua za kinga na udhibiti za nchi hizo katika kukabiliana na virusi hivyo. Imesema kama hali ikizidi kuwa mbaya, serikali ya China itachukua hatua za lazima za kuwarudisha nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako