• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wagonjwa zaidi ya elfu moja wapona na kuondoka kutoka hospitali kubwa kabisa ya muda mjini Wuhan

    (GMT+08:00) 2020-03-02 09:57:08

    Mamlaka ya mji wa Wuhan imesema hadi kufikia jumapili hospitali kubwa kabisa ya muda iliyo na vitanda vingi mjini Wuhan, mkoani Hubei ambako ni kiini cha mlipuko wa virusi vya Korona nchini China, imewatibu wagongjwa zaidi ya 1,000.

    Kwa mujibu wa makao makuu ya kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi mkoani Hubei, hospitali ya muda ya Jianghan iliyojengwa kwenye Kituo cha maonyesho cha kimataifa cha Wuhan, ina vitanda 1,564 na wafanyakazi zaidi ya 1,100, na ilianza kuwapokea wagonjwa tarehe 5 Februari.

    Hadi kufikia Ijumaa, mji wa Wuhan ulikuwa na hospitali 16 za muda zenye vitanda zaidi ya 5,000 zilizojengwa kwenye majumba ya kufanyia mazoezi, vituo vya maonyesho, na majengo mengine makubwa, ili kukabiliana na uhaba wa vitanda vya wagonjwa.

    Aidha makao makuu hayo pia yamesema hadi kufikia Jumamosi mkoa wa Hubei umepata mchango wa dola za kimarekani zaidi ya bilioni 1.86, pamoja na vifaa zaidi ya milioni 92, vikiwemo mask, nguo, na miwani za kujikinga dhidi ya virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako