• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumia Data Kubwa katika udhibiti wa mipaka kuzuia maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-02 10:00:08

    Ofisa wa Mamlaka ya Uhamiaji ya Taifa ya China NIA Bw. Liu Haitao, amesema uchanganuzi wa Data Kubwa (Big Data) umetumiwa katika udhibiti wa mipaka ili kuzuia kuingia kwa wagonjwa wa COVID-19 kutoka nje ya nchi.

    Bw. Liu amesema matokeo ya uchanganuzi wa Data Kubwa yatatumika kwa pamoja na maafisa wa karantini wa forodha ili kuwafanya wapate muda mwingi wa kushughulikia karantini kwa ufanisi. Pia ameeleza kuwa kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kutoka nje ya China imekuwa kazi kuu kwa mamlaka hiyo kwa sasa.

    Ameongeza kuwa mamlaka hiyo itaimarisha ushirikiano wa kimataifa na nchi na sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa huo, kupitia udhibiti wa mipaka na upashanaji wa habari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako