• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Abiria kutoka Meli ya Diamond Princess iliyowekwa karantini athibitishwa kuambukizwa COVID-19 huko Taiwan

    (GMT+08:00) 2020-03-02 10:23:34

    Kwa mujibu wa idara ya usimamizi wa magonjwa ya kuambukiza ya Taiwan, abiria aliyetoka meli ya abiria ya Diamond Princess iliyowekwa karantini nchini Japan amethibitishwa kuwa mgonjwa wa 40 wa nimonia ya COVID-19 kisiwani Taiwan. Mgonjwa huyo mpya ni mwanamke mwenye umri wa miaka zaidi ya 70 anayeishi kaskazini mwa Taiwan, ambaye alipanda meli hiyo Januari 20 na kutambuliwa kuambukizwa virusi hivyo Februari 15 baada ya meli hiyo kuwekwa karantini huko Yokohama, Japani tangu Februari 4, hata hakuonesha dalili yoyote. Alilazwa hospitalini nchini Japani kutoka Februari 16 na kurudi Taiwan Februari 26 na kuthibitishwa kuambukizwa baada ya upimaji wa mara tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako