• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bandari kavu kujengwa Arusha.

    (GMT+08:00) 2020-03-02 18:43:05

    Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iko mbioni kujenga bandari kavu ya muda mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuhifadhi makontena yanayotoka nje ya nchi hususani kahawa inayotoka Arusha na Kilimanjaro kwenda nje ya nchi yatahifadhiwa hapo.

    Aidha, Bandari Kavu ya Arusha itajengwa eneo la Malula wilayani Arumeru ambapo mizigo yote itahifadhiwa hapo.

    Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe jijini Arusha alipokuwa akikagua ukarabati wa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 86 kutoka Moshi hadi Arusha.

    Naye Mhandisi wa Reli anayesimamia ukarabati huo kuanzia Tanga, Shadrack Massawe, amesema ukarabati wa reli hiyo uko katika hatua za mwisho na umekamilika kwa zaidi ya asilimia 94.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako