• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza kuongeza uratibu wa kimataifa katika kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-02 19:09:47

    Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi ametoa makala kwenye jarida la Qiushi la Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na kusema, mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 umeonesha kuwa, mustakabali wa kila nchi unahusiana katika kipindi cha utandawazi.

    Ameongeza kuwa, kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja ni njia pekee mwafaka kwa maendeleo ya jami ya binadamu, na China itapanua ushirikiano wa pande mbili na pande mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huo.

    Ameongeza kuwa, China itaendelea kudumisha mawasiliano mazuri na Shirika la Afya Duniani (WHO), kutafuta na kujenga mfumo wa kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa pamoja, kubadilishana habari, hatua zenye ufanisi na mafanikio ya utafiti na kuongeza utafiti wa pamoja wa dawa na chanjo dhidi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.

    Bw. Wang pia amesema, hivi sasa, China imebeba wajibu wake ikiwa nchi kubwa duniani, na kutoa misaada kwa nchi nyingi zinazokumbwa na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako