• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tishio la COVID-19 laongezeka duniani huku China ikiahidi kufanya ushirikiano wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-03-02 19:11:52

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, wakati maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 yanaenea zaidi duniani, ugonjwa huo ni changaomto inayokabili binadamu wote, na China itaendelea kufuata wazo la jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu, na kufanya ushirikiano wa kimataifa kwa hatua madhubuti, ili kulinda usalama wa afya wa kikanda na kimataifa.

    Hivi karibuni, maambukizi ya COVID-19 yameongezeka kwa kasi katika nchi kadhaa ikiwemo Iran na Italia. Zhao amesema, China inapenda kutoa misaada kadiri iwezavyo kwa nchi hizo, na kuongeza mawasiliano na kubadilishana nao uzoefu.

    Habari nyingine zinasema, mkutano wa 53 wa kamati ya mawaziri wa afya wa nchi za Kiarabu uliofanyika hivi karibuni umeipongeza na kuiunga mkono China kwa juhudi zake za kupambana na COVID-19. Zhao amesema tangu kutokea kwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini China, nchi za Kiarabu zimeinga mkono China kithabiti, hali iliyoonesha urafiki wa jadi na uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako