• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kurekebisha hatua za kinga na udhibiti kwa wageni wanaoingia kwa mujibu wa mabadiliko ya hali ya maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-02 19:12:34

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, China itarekebisha hatua za kinga na udhibiti kwa wageni wanaoingia kwa mujibu wa mabadiliko ya hali ya maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19.

    Hivi sasa sehemu mbalimbali za China zimechukua hatua kulingana na sheria za China kwa wageni wanaotoka nchi na sehemu zinazoathiriwa vibaya na COVID-19 ikiwemo kuwapima joto, kuwataka wakae nyumbani bila kutoka au kuwapelekea katika hoteli kwa ajili ya kufuatiliwa kwa afya zao kwa muda wa siku 14.

    Akizungumzia hatua hizo, msemaji huyo amesema sio tu zinahitajika katika kukinga na kudhibiti maambukizi ya COVID-19, bali pia zinaweza kuzuia kuenea kwa virusi kati ya nchi na nchi, na ni muhimu kwa pande zote za China na nchi za kigeni katika vita dhidi ya virusi. Pia amesema China inawatendea raia wake na wa kigeni kwa usawa, kuchukua hatua bila tofauti, pia kuzingatia ufuatiliaji wao halali na kutoa mahitaji na msaada wa lazima. Zhao ametoa wito kwa watu wanaokuja China kutoka nchi zenye hali mbaya ya maambukizi ya COVID-19 kuelewa na kufuata hatua husika ili kujikinga na hatari ya kuambukizwa virusi, na kulinda afya na usalama wao wenyewe na watu wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako