• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la China lapeleka vifaa vya matibabu na mahitaji ya kila siku mjini Wuhan

    (GMT+08:00) 2020-03-02 19:13:41

    Jeshi la ulinzi la China limechukua nafasi muhimu katika upatikanaji wa vifaa vya matibabu na mahitaji ya kila siku katika mji wa Wuhan, ikiwa ni sehemu ya juhudi za nchi hiyo kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19.

    Mpaka kufikia jumatatu, askari 260 na magari 130 kutoka Kamandi Kuu ya Jeshi la Ukombozi la China lilipewa jukumu la kusafirisha tani 8,500 za mahitaji ya kila siku na seti 23,600 za mavazi ya kujilinda na vifaa vingine mjini Wuhan, ambako ni chimbuko la mlipuko wa COVID-19.

    Wakati huohuo, jeshi la China limeahidi kufanya ushirikiano wa kijeshi na kufanya kazi na majeshi ya nchi nyingine ili kupambana na matishio ya afya ya umma ikiwemo mlipuko wa virusi vya korona.

    Takwimu zinaonesha kuwa karibu vitanda 3,000 vimewekwa katika hospitali 63 zenye hadhi ya kijeshi zilizotengwa kwa ajili ya kuhudumia watu waliopata maambukizi ya virusi vya korona. Ofisa afya kutoka idara ya ugazi iliyo chini ya Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, Chen Jingyuan amesema, zaidi ya wahudumu wa afya 10,000 wa jeshi la China wako msatri wa mbele katika kupambana na mlipuko wa virusi hivyo.

    Habari nyingine zinasema msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Wu Qian amesema, China itaharakisha utoaji wa sheria kuhusu usalama wa viumbe, na kukamilisha mfumo husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako