• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na kundi la Taliban yatekelezwe kwa mafanikio

    (GMT+08:00) 2020-03-02 19:19:05

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, Marekani na kundi la Taliban zinapaswa kutimiza amani nchini Afghanistan kwenye msingi wa makubaliano yao yaliyosainiwa jumamosi iliyopita mjini Doha, Qatar.

    Amesema China inaunga mkono na kupenda kutoa misaada kwa kuhimiza mchakato wa maafikiano ya amani wa Afghanistan, unaoongozwa na kudhibitiwa na watu wa Afghanistan. Vikosi vya nchi za nje nchini Afghanistan vinapaswa kuondoka kwa utaratibu ili kuhakikisha hali nchini humo inaendelea kwa utulivu, na kuzuia ukosefu wa usalama, hasa kuenea kwa makundi ya kigaidi. Pia China inataka jumuiya ya kimataifa iendelee kuunga mkono na kujiunga na mchakato wa ukarabati wa amani nchini Afghanistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako