• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yapokea vifaa vya matibabu ya virusi vya korona kutoka WHO

    (GMT+08:00) 2020-03-03 09:08:56

    Shirika la habari la Iran IRNA, limesema Iran imepokea vifaa vya matibabu ya virusi vya korona kutoka Shirika la afya duniani (WHO).

    Shirika hilo limesema, vifaa hivyo vyenye uzito wa tani 7.5 vilisafirishwa kwa ndege ya kijeshi ya Falme za Kiarabu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini, Tehran. Vifaa hivyo ni pamoja na dawa, vifaa vya upimaji, glavu, na mask za kujikinga.

    Aidha kikundi cha watu 6 ambao ni pamoja na madaktari, wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza, na wataalamu wa maabara wamewasili Tehran kuisaidia Iran kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako