• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa vifaa vya upimaji kwa Iraq ili kuisaidia kupambana na virusi vya korona

    (GMT+08:00) 2020-03-03 09:09:13

    Balozi wa China nchini Iraq Bw. Zhang Tao, amesema China itatoa vifaa vya upimaji kwa Iraq, ili kuisaidia kupambana na mlipuko wa virusi vya korona.

    Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa China nchini Iraq imesema, balozi Zhang ametangaza habari hiyo alipokutana na naibu waziri wa mambo ya nje wa Iraq anayeshughulikia mambo ya siasa Bw. Abdul Karim Mustafa, ambapo wamebadilishana maoni kuhusu ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya virusi vya korona.

    Taarifa hiyo imesema, vifaa vya upimaji vitakavyotolewa na China vinatosha kutambua maambukizi 1,000 kati ya watu wanaoshukiwa kuambukizwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako