• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Carlo Ancelotti awa kocha wa kwanza kurambwa kadi nyekundu

    (GMT+08:00) 2020-03-03 12:05:46

    Bosi wa Everton Carlo Ancelotti ameshtakiwa na FA baada ya kupewa kadi nyekundu na kutolewa nje ya kiwanja walipotoka sare dhidi ya Manchester United. Muitaliana huyo alimwendea mwamuzi Chris Kavanagh kikipigwa kipenga cha mwisho baada ya goli la dakika za majeruhi la Dominic Calvert-Lewin kuamuliwa kuwa sio goli kwani aliotea. Ancelotti hatapata adhabu ya kufungiwa bali atatozwa faini ya £8,000 kama atakubali makosa kabla ya siku ya mwisho Alhamis. Kiasi hicho kinaweza kupanda hadi£12,000 kama atakata rufaa na kushindwa. Baada ya sare ya 1-1 katika uwanja wa Goodison Park, Ancelotti mwenye miaka 60 amesema kwamba hakumvunjia heshima Kavanagh ambaye uamuzi wake wa awali wa kuruhusu goli katika dakika za majeruhi ulibadilishwa na VAR kwasababu mchezaji wa Everton Gylfi Sigurdsson aliotea mbele ya mlinda mlango wa United David de Gea. Hata hivyo Ancelotti amesema baadaye alikuwa na mazungumzo ya faragha ambapo aliongea na mwamuzi kwa upole. Ingawa bosi wa Toffees ni kocha wa kwanza wa Ligi ya Premier kupewa kadi nyekundu, sheria hiyo imeanzishwa msimu huu na Bodi ya Shirikisho la Soka Kimataifa ili kuweka wazi vitendo kama hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako