• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Korea Kusini atangaza vita dhidi ya COVID-19 wakati maambukizi yakizidi 5,000

    (GMT+08:00) 2020-03-03 20:06:28

    Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ametangaza vita dhidi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19) wakati idadi ya kesi za maambukizi nchini humo ikipita 5,000, hivyo kuziweka taasisi za serikali hiyo katika hali ya tahadhari.

    Akizungumza katika mkutano wa kila wiki wa Baraza la Mawaziri, rais Moon ametangaza kutenga dola za kimarekani bilioni 25 zitakazotumika moja kwa moja kushughulikia maambukizi ya virusi vya korona. Mpaka kufikia saa kumi jioni leo, idadi ya maambukizi mapya imefikia 374, na kufanya idadi ya jumla ya watu walioambukizwa kuwa 5,186, na watu 29 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

    Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema, askari wengine wawili na raia anayefanya kazi jeshini wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya korona, hivyo kufanya idadi ya jumla ya wanajeshi waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo kufikia 31.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako