• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Viwango vya riba kwa benki za biashara vyapungua Uganda

    (GMT+08:00) 2020-03-03 20:18:39

    Viwango vya riba za benki za biashara nchini Uganda vimepungua hadi wastani wa asilimia 19.

    Mkurugenzi wa utafiti kwenye Benki kuu ya Uganda Dk Adam Mugume amesema riba ya benki hiyo ya asilimia 9 kwa mwezi wa Februari, kimeshinikiza kushuka kwa viwango vya mikopo ya benki za biashara kwa asilimia 4.

    Kwa mujibu wa Benki Kuu, viwango vya mikopo ya benki za biashara vimepungua hadi asilimia 19 mwezi Januari kutoka wastani wa asilimia 20.5 katika robo ya mwisho ya mwaka jana.

    Mugune pia amesema ndani ya serikai wamepata ogezeko ikilinganishwa na mwezi Disemba 2019.

    Soko la mikopo ya sekta binafsi liliongezeka kwa asilimia 1.8 kutoka Shilingi trilioni 15 mwezi Novemba hadi shilingi trilioni 15.

    Na viwango vya mikopo ya ya dola za kimarekani na vilipungua hadi asilimia 6.5 kutoka asilimia 7 ya robo ya mwisho ya mwaka 2019.

    Benki Kuu imedumisha sera ya kifedha mwaka jana, ambayo imechochea utendaji kwenye masoko ya kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako