• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Serikali ya Rwanda kurekebisha sera za uwekezaji

    (GMT+08:00) 2020-03-03 20:19:21

    Serikali ya Rwanda inapanga kurekebisha sera zake ili kukuza miradi ya pamoja ya uwekezaji, haswa katika sekta ya viwanda na huduma.

    Mpango huo ni sehemu ya maazimio ya mkutano wa Uongozi wa Kitaifa.

    Mkutano huo wa 17 ulikuwa na maazimio 16 manne yakiwa yanahusu sekta binafsi.

    Mkurugenzi Mkuu wa Biashara na Uwekezaji katika Wizara ya Biashara na Viwanda, Tony Kajangwe, alisema serikali ina mpango wa kuendelea kufanya kazi na wadau mbali mbali kurekebisha sera husika na kuweka utaratibu wa kusaidia sekta binafsi ili kufanikisha malengo ya serikali .

    Miongoni mwa mapendekezo ni kukagua sera zinazohusiana na udhibiti na usimamizi wa fedha, kwa msaada wa taasisi ambazo zitasaidia moja kwa moja katika kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa mikopo kutoka taasisi za kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako