• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Misri akagua hali ya usalama pamoja na maofisa wa kijeshi

    (GMT+08:00) 2020-03-04 09:37:36

    Jeshi la Misri limetoa taarifa kuwa rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri amejadiliana na maofisa waandamizi wa kijeshi kuhusu maendeleo ya usalama nchini humo. Mkutano huo umehudhuriwa na waziri wa ulinzi, kamanda mkuu wa jeshi Mohamed Zaki na mnadhimu mkuu Mohamed Farid. Rais Al Sisi amearifiwa hali ya jumla ya usalama nchini Misri pamoja na njia za usalama na mipango iliyotekelezwa na jeshi hilo na kuwasaka na kuwakamata magaidi wanaojaribu kuivuruga nchi hiyo hasa katika eneo la Sinai Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako