• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Daniel Sturridge atemwa na klabu yake Trabzonspor kwa kuhusika kwenye kamari

    (GMT+08:00) 2020-03-04 10:11:40

    Klabu ya Trabzonspor ya Uturuki imemtema mshambuliaji wake, Daniel Sturridge. Sturridge ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Liverpool, ametemwa baada ya kubainika kuwa ndugu yake amecheza kamari wakati yeye akijiunga na timu hiyo. Ndugu yake huyo ambaye imeelezwa ni kaka yake, alicheza kamari na kushinda mamilioni ya fedha akitabiri yeye Sturridge atajiunga na klabu hiyo ya Uturuki. Adhabu ya Trabzonspor, inafuatia adhabu ya FA na Fifa ambazo zimemfungia hadi Juni kutokana na kitendo hicho. Kawaida Fifa, FA na mashirikisho mengine ya soka yanazuia wanasoka kushiriki kwa aina yoyote katika masuala ya kamari. Awali Sturridge alikata rufaa lakini akashindwa kwa mara nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako