• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kamworor kuongoza kikosi cha nusu marathon Poland

    (GMT+08:00) 2020-03-04 16:11:59

    Bingwa mtetezi Geoffrey Kamworor na mshindi wa nishani ya shaba katika mbio za kilomita 21 duniani, Pauline Kaveke wataongoza kikosi cha Kenya katika mashindano ya 24 ya Nusu Marathon ya Dunia Machi 29 mjini Gdynia, Poland. Shirikisho la Riadha la Kenya (AK) limemteua Kamworor ambaye atawania ubingwa wa mbio hizo kwa mara ya nne mfululizo kuwa kiongozi wa timu ya wanaume inayomjumuisha pia Kibiwott Kandie. Kabla ya kutua UAE alikotawala Ras Al Khaimah Half Marathon Februari 21, Kandie alimshinda Kamworor Februari 15 mjini Ngong na kunyanyulia kikosi chake cha KDF medali ya kwanza ya Mbio za Nyika za Kitaifa baada ya miaka 17. Kamworor ambaye ni bingwa wa dunia katika Nusu Marathon, alitawazwa mshindi wa mbio hizo kwa mara ya tatu 2018 jijini Valencia, Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako