• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasambazaji wa gesi watakiwa kupima kabla ya matumizi

    (GMT+08:00) 2020-03-04 19:06:50

    Wafanyabiashara wa gesi ya kupikia (LPG), Kanda ya Ziwa, hususani wasambazaji wametakiwa kuhakikisha mitungi ya gesi inakuwa na uzito sahihi na wafanyabiashara kuzingatia sheria, kanuni, utaratibu na usalama.

    Akizungumza katikia warsha ya kuwajengea uwezo wasambazaji wa gesi kutoka mikoa saba nchini humo, meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) Kanda ya Ziwa, George Mhina, amesema wamefundisha namna ya kuhifadhi mitungi sehemu za kivuli na kuweka mita nane kutoka eneo la kupikia.

    Aliwataka wasambazaji hao, kuwa na vifaa vya kupimia uzito na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kinyume chake adhabu kali itafuata kwa kuwa Ewura inafanya ukaguzi wa mara kwa mara na sheria inawapa mamlaka ya kutoza faini.

    Pia alisema, matumizi ya gesi ya kupikia ni muhimu kwa kuwa inatunza mazingira pia gharama zake ni nafuu.

    Amesisistiza kuwa Ewura itaendelea kushirikiana na kampuni za LPG kuwabaini wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa kuchukua hatua stahiki na hivi karibuni itaanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya LPG wasambazaji ambao hawana leseni ya mamlaka hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako