• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara yatahadharisha mvua kubwa kunyesha mwezi huu

    (GMT+08:00) 2020-03-04 19:07:59

    Wakenya Hususan wakulima na wafanya biashara wametakiwa kujiandaa kwa ajili ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi kuanzia mwezi huu wa Machi.

    Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ilisema kuwa kiwango cha mvua kitakuwa kikubwa zaidi Aprili katika maeneo yote ya nchi isipokuwa Pwani ambapo kiwango kitakuwa cha juu zaidi Mei.

    Mkurugenzi wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa, Bi Stella Aura alisema kuwa mvua kubwa inatarajiwa katika maeneo ya Magharibi, Pwani, Kaskazini Mashariki, Kati na upande wa Mashariki.

    Hata hivyo, maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Kenya, kama vile Turkana, yatakuwa na kiwango cha kawaida cha mvua.

    Kulingana na Bi Aura, mvua kubwa inatarajiwa kuanzia wiki hii katika maeneo ya Pwani, Magharibi, nyanda za Kati na Bonde la Ufa. Maeneo mengine ya nchi yataanza kupokea mvua wiki ya tatu na nne ya mwezi huu.

    Alisema kuwa maeneo ya Kati na magharibi mwa Kenya yalipokea kiasi kikubwa cha mvua Februari.

    Amesema taarifa hiyo inalenga kuwafanya wakulima na wafanyabiashara kujiandaa kikamilifu kabla ya kuanza biashara zao huku wakulima wakitakiwa kujipanga katika upanzi wa mazao..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako