• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyanza kuanza ununuzi mazao ya kimkakati

    (GMT+08:00) 2020-03-04 19:08:21

    Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mwanza (Nyanza 1984 Limited), kinatarajia kuanzisha ununuzi wa mazao ya kimkakati ya biashara dengu na choroko, kupitia mfumo wa ushirika wa stakabadhi ghalani.

    Kaimu Meneja Mkuu wa chama hicho, Martha Ndeto, alisema kuwa chama hicho kitakuwa kinakusanya mazao hayo kupitia vyama vya msingi vya ushirika vya mazao (Amcos).

    Ndeto alisema serikali inajitahidi kuboresha vyama vya ushirika lengo likiwa wakulima waweze kuuza mazao yao kwa bei nzuri yenye faida pamoja na kuepuka kupunjwa bei na kampuni binafsi zinazonunua mazao hayo.

    Alisema wakulima wamekuwa wakiuza mazao hayo kiholela kwa kampuni binafsi kwa kutumia visado badala ya kupima kwenye kilo, jambo ambalo linawafanya wasinufaike na kilimo cha mazao ya kimkakati ya biashara.

    Alizitaka mamlaka zote zinazohusika na usimamizi wa mazao ya wakulima ya kimkakati mkoani Mwanza kushiriki kikamilifu katika kutimiza wajibu wao, ili kusaidia kuwainua wakulima kiuchumi, kwani mfumo utakaotumika hivi sasa utazinufaisha pia Amcos pamoja na Nyanza katika kukuza uchumi wake.

    Alisema Amcos hivi sasa zimeshindwa kujiendesha zenyewe katika utekelezaji wa majukumu yake, kutokana na kutolipwa fedha za ushuru wa pamba, na baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao hilo tangu msimu uliopita 2019 ulioanza Mei.

    Ndeto alifafanua kuwa wakulima mwaka huu mkoani Mwanza, wameshindwa kulima pamba kwa wingi kama mwaka jana kutokana na kuwapo mvua nyingi ambayo pamba haiwezi kustawi katika maeneo mengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako