• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vya Marekani vyafanya shambulizi la kwanza dhidi ya kundi la Taliban baada ya makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2020-03-04 19:20:44

    Vikosi vya Marekani nchini Afghanistan vimefanya shambulizi la anga kuunga mkono vikosi vya usalama vya Afghanistan katika mkoa wa kusini wa Helmand hii leo, ikiwa ni shambulizi la kwanza baada ya Marekani na kundi la Taliban kusaini makubaliano ya amani.

    Msemaji wa kikosi cha Marekani nchini Afghanistan Kanali Sonny Legetta amesema kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, shambulizi hilo lilifanywa dhidi ya wapiganaji wa kundi la Taliban katika wilaya ya Nahr-e-Saraj baada ya wapiganaji hao kushambulia kituo cha ukaguzi cha jeshi la ulinzi na usalama la Afghanistan. Amesema jana pekee, kundi la Taliban lilifanya mashambulizi 43 katika vituo vya ukaguzi vya jeshi la ulinzi na usalama la Afghanistan mkoani Helmand.

    Februari 29, mkuu wa kisiasa wa kundi la Taliban Mullah Abdul Ghani Baradar na mjumbe maalum wa Marekani kuhusu Afghanistan Zalmay Khalilzad walisaini makubaliano ya amani mjini Doha, Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako