• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yapokea misaada ya kimataifa ya kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-05 09:47:16

    Iran imepokea misaada ya kimataifa kuisaidia kupambana na nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vipya vya korona, wakati nchi nyingi zaidi za Mashariki ya Kati zikichukua hatua zaidi katika kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo Bw. Abbas Mousavi, amesema Shirika la afya duniani WHO limesafirisha vitu vingi vya misaada nchini humo. Msaada wa kwanza wa kibinadamu kutoka Ufaransa ulikabidhiwa kwa Wizara ya afya na matibabu ya Iran. Mbali na hayo, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, China, Uturuki na Austria pamoja na nchi za Ulaya, zimetoa vifaa vya matibabu kwa Iran kuisaidia kupambana na ugonjwa huo.

    Siku hiyo rais Hassan Rouhani wa Iran alisema kwenye mkutano wa baraza la mawaziri kuwa, kama Marekani inataka kuisaidia Iran kupambana na ugonjwa huo kwa dhati, inatakiwa kuondoa vikwazo vya kuuzia Iran vifaa vya matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako