• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema kazi ya kuzuia na kudhibiti COVID-19 lazima ipewe kipaumbele na nchi zote

    (GMT+08:00) 2020-03-05 10:07:10

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani Bw. Tedros Ghebreyesus amesema hali ya janga la dunia la nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vipya vya korona inazidi kuwa ngumu, na kazi ya kuzuia na kudhibiti virusi hivyo lazima iwe kipaumbele kwa nchi zote, na kila nchi inapaswa kujiandaa kukabiliana na kusambaa kwake katika jamii.

    Katika mkutano wa kila wiki kuhusu mlipuko wa COVID-19, Bw. Tedros amesema WHO imezingatia maambukizi kati ya nchi na sehemu, maambukizi ya kijamii yametokea katika baadhi ya maeneo, lakini maambukizi mengi bado yanaweza kufuatiliwa.

    Kutokana na uzoefu wa China katika kuzuia na kudhibiti virusi hivyo, Bw. Tedros ameongeza kuwa WHO inapendekeza kila nchi ichukue hatua kamili na madhubuti haraka iwezekanavyo, na kutaka nchi zote kuimarisha uelimishaji, kupanua maeneo ya usimamizi, kuwatambua, kuwaweka karantini na kuwatunza wagonjwa waliothibitishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako