• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA:Victor Wanyama apewa mkono wa kwaheri Tottenham na kuelekea Montreal Impact

    (GMT+08:00) 2020-03-05 10:23:52

    Tottenham Jumatano, Machi 4, ilitangaza kuwa imekubaliana na Montreal Impact kumuuza Victor Wanyama. Ofa hiyo itamshuhudia kiungo huyo wa kati akiondoka kwenye klabu hiyo ya London. Wanyama alitumia mtandao wa kijamii kuandika ujumbe kwa mashabiki wake wa Spurs huku akiwashukuru kwa kumuunga mkono wakati wake katika klabu hiyo. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye miaka 28, alishindwa kuficha furaha yake kwa kufaulu kupata mazingira mapya Montreal Impact. Huku akijitambulisha kama simba, kiungo huyo wa zamani wa Celtic alionyesha imani ya kusaidia klabu hiyo ya Canada kufikia kilele. Kiranja huyo wa Harambee Stars alikuwa katika klabu ya Tottenham kwa miaka mitatu, baada ya kujiunga nao akitokea Southampton mwaka 2016. Licha ya kuanza maisha yake kwa kung'aa na Lilywhites, makali yake yalipungua na kumpelekea kushuka kimchezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako