• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Tottenham Hotspurs waaga michuano ya FA Cup baada ya kuondolewa na Norwich City

    (GMT+08:00) 2020-03-05 10:24:29

    Klabu ya Tottenham Hotspurs wameaga michuano ya FA Cup baada ya kuondolewa kwa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Norwich City kutokana na mechi hiyo iliyopigwa kwa dakika 120 kumalizika kwa sare ya kufungana moja moja kama ilivyokuwa katika mchezo wa kwanza. Jose Mourinho akiwa na kikosi chake cha Tottenham amekuwa na wakati mgumu kutokana na timu yake kuondolewa mapema, ushindi huo wa Norwich unamfanya acheze na mshindi wa mechi ya Derby County dhidi ya Man United. Michezo ya robo fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kati ya March 20 na 22, timu zilizofuzu kucheza hatua ya robo fainali ni Man City, Leicester, Norwich, Arsenal, Sheffield United, Newcasle United na Chelsea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako