• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Bingwa wa Olimpiki Ruth Jebet apigwa marufuku kwa miaka minne

    (GMT+08:00) 2020-03-05 10:26:50

    Mshika rikodi ya dunia wa zamani wa mbio za kuruka viunzi mita 3,000 Mkenya Ruth Jebet ambaye amehamia Bahrain amepigwa marufuku kwa miaka minne kushiriki riadha kuanzia Februari 4, 2018. Jebet, ambaye ni bingwa wa Olimpiki ya Rio 2016 mita 3,000 kuruka viunzi, sasa atatumikia rasmi marufuku hiyo baada ya kushindwa kesi yake ya rufaa kwenye kitengo cha maadili ya wanariadha. Jebet, mwenye miaka 23, alianza kusimamishwa tangu Februari 2018 baada ya sampuli ya mkojo wake kupimwa na kugundulika kutumia Erythropoietin (Epo) michezoni ambayo imepigwa marufuku. Sampuli hiyo ilichukuliwa walipokuwa kwenye mashindano Disembea 1, 2017 huko Kapsabet. Jebet alikiri kutumia (Epo) lakini amesema sio kwa makusudi na kumlaumu msimamizi wake kwa tatizo hilo, kwani amesema amekuwa akipewa vidonge na sindano lakini kwaajili ya matibabu na si kwa kusisimua misuli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako