• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Korea Kusini na Korea Kaskazini wapeana barua za salama

    (GMT+08:00) 2020-03-05 17:58:06

    Ikulu ya Korea Kusini leo imesema rais wa nchi hiyo Moon Jae-in amebadilishana barua na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un.

    Katibu wa ngazi ya juu wa ikulu ya Korea Kusini Yoon Do-han amesema, Bw. Kim Jong Un jana alimtumia rais Moon Jae-in barua, akitoa salamu zake kwa wananchi wa Korea Kusini wanaopambana na mlipuko wa virusi vya korona, na kusema anaamini kuwa Korea Kusini inaweza kushinda vita hiyo.

    Kwa upande wake, rais Moon amemtumia Kim barua ya shukrani kwa ufuatiliaji wake.

    Mpaka kufikia Alhamisi saa kumi jioni, Korea Kusini imeripoti kuwa jumla ya watu 6,088 walioambukizwa virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako