• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GOLF: TANAPA yaendelea kuipiga tafu golf

    (GMT+08:00) 2020-03-05 18:19:26

    Shirika ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kudhamini mashindano ya golf ya Klabu ya Lugalo ambayo yamepangwa kufanyika Machi 14 – 15 mwaka huu kwenye viwanja vya klabu hiyo jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo mwaka huu yamepewa jina la TANAPA Lugalo Golf na yanatarajia kushirikisha zaidi ya wachezaji 100 ambao watakuwa katika madaraja mbalimbali. TANAPA inachukua nafasi hiyo kuendelea kutangaza hifadhi za Taifa kupitia michezo, na pia kukusanya wachezaji mbalimbali pamoja ili kubadilishana uzoefu wa mchezo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako