• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Habari za uongo kuhusu Corona zaathiri biashara katika sekta ya usafiri nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2020-03-05 20:12:07

    Usambazaji wa habari za uongo mitandaoni kuhusu mkurupuko wa virusi vya korona nchini Kenya umewatia hofu wasafiri wanaonuia kuja Kenya.

    Haya ni kwa mujibu wa Chama cha Maajenti wa Usafiri Nchini – Kenya Association of Travel Agents (Kata) .

    Katika kikao na waandishi wa habari hii leo jijini Nairobi,Chama hicho kinasema jumbe hizo zimechangia katika kuwapotosha watalii kutoka nchi mbalimbali na hivyo kusababisha hasara kubwa katika sekta hiyo.

    Mwenyekiti wa chama cha Kata Mohammed Wanyoike ametoa wito kwa wasafiri wanaoinuia kuzuru nchi ya Kenya kuwasiliana moja kwa moja na Chama hicho ili kupata habari za ukweli kuhusu hali ilivyo nchini Kenya.

    Wamyoike alisema sekta ya usafiri ndio iliyoathirika zaidi kimataifa na mkurupuko wa virusi vya COVID-19.

    Wakati huo huo Bw Wanyoike alisema kuna matumaini kuwa hali ya kawaida itarejea katika nusu ya pili ya mwaka ambapo wanatarajia wageni wengi kuwasili nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako