• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Wataalamu watoa wito wanawake kujumuishwa katika sekta za biashara na fedha

    (GMT+08:00) 2020-03-05 20:12:31
    Huku siku ya Kimataiafa ya Wanawake Duniani ikikaribia,wataalamu nchini Rwanda wanashauri uundaji wa mikakati endelevu ili kuwahusisha wanawake wengi zaidi katika sekta za biashara na fedha.

    Kauli jiyo ilitolewa wakati wa kongamano lililoleta pamopja Wizara ya Jinsia na Ukuzaji wa Familia,Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu nchini Rwanda na Wataalamu jana jijini Kigali.

    Chini ya kualimbiu "Uzalishaji na matumizi ya takwimu za Jinsia" ,data zilizowasilishwa zilionyesha kuwa licha jitihada na maboresho yaliyofanywa katika miaka iliyopita,wanawake bado hawajajumuishwa katika sekta za biashara na fedha kama wanaume.

    Utafiti wa biashara wa mwaka 2018 ulionyesha kuwa nchini Rwanda,asilima 70 ya wafanyakazi katika ajira rasmi ni wanaume,na asilimia 29 ni wanawake.

    Mojawapo ya suluhisho lililopendekezwa wakati wa kongamano hilo ni kuhimiza sekta binafsi na mashirika ya kijamii kuchukua jukumu la kusaidia wanawake kujiunga na biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako