Ripoti ya Mhasibu Mkuu wa serikali nchini Uganda imesema kuwa tathmini ndogo ya malipo ya mirahaba katika sekta ndogo ya madini imesababisha ukosefu wa mapato.
Kulingana na Ripoti ya Mhasibu Mkuu wa Serikali ya mwaka 2018/19,Wizara ya Nishati na Madini ilikusanya Shs10.5b katika mirahaba ya madini.
Hakiki za Mamlaka ya Mapato ya Uganda zinaonyesha kuwa sekta ndogo ya madini naweza kuzalisha zaidi ya Shs70.2b katika kiwango cha asilimia 5 haswa kutoka dhahabu,tantalum na tungsten.
Mashirika ya kijamii yameitaka serikali kuchukua hatua zinazohitajika ili kuziba pengo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |