Mwakilishi maalumu wa wizara ya mambo wa China anayeshughulikia haki za binadamu Bibi Liu Hua amesema hakuna ugaidi "mzuri" au ugaidi "mbaya" duniani, ugaidi ni ugaidi tu na haipaswi kuwa na vigezo viwili kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.
Akiongea kwenye mjadala wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuhimiza na kulinda haki za binadamu wakati wa mapambano dhidi ya ugaidi, kwenye mkutano wa 43 wa baraza la haki za binadamu la umoja huo, Bibi Liu amesema ugaidi ni adui wa binadamu wote.
Amesema kwa sasa mapambano dhidi ya ugaidi duniani yamekuwa na utatanishi na makali, jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na wimbi jipya la shughuli za kigaidi, ambalo hutoa tishio kubwa kwa usalama na utulivu wa kikanda na kimataifa, kwa hiyo pande zote zinapaswa kuchunguza uwiano kati ya ugaidi na ulinzi wa haki za binadamu, kuzuia ukiukaji wa haki na maslahi ya raia na mashirika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |