• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Eric Dier aruka uzio kwenda jukwaani kuzichapa na shabiki baada ya kutukanwa

    (GMT+08:00) 2020-03-06 10:25:30

    Kiungo wa kimataifa wa Uingereza Eric Dier jana aliruka uzio kwenda jukwaani kutaka kuzichapa na shabiki. Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa mashindano ya Kombe la FA ambao Tottenham Hotspurs ilitupwa nje kwa kufungwa mabao 3-2 kwa penalti baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Norwich City. Kocha wa Spurs Jose Mourinho alisema kiungo huyo alitolewa lugha kali na shabiki. Dier alikwenda kwa kasi jukwaani na kumvaa shabiki huyo kabla ya maofisa usalama kumzuia. Dier aliyecheza mechi 40 za England na alishindwa kuisaidia Spurs kusonga mbele katika mashindano hayo baada ya kipa wa Norwich Tim Krul kuokoa panalti mbili. Norwich inashika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu England na matokeo hayo yamewachukiza mashabiki wa Spurs. Alisema lugha ya maudhi iliyotolewa na shabiki huyo ilikuwa ya kumchukiza mchezaji huyo kwa kuwa familia yake ilikuwa uwanjani. Katika mechi nyingine, Leicester City iliichapa Birmingham bao 1-0, pia Manchester City iliilaza Sheffield Jumatano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako