• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Ronaldinho na kaka yake wakamatwa kwa kuwa na pasipoti feki

    (GMT+08:00) 2020-03-06 10:25:44

    Mchezaji mkongwe wa Brasil, Ronaldinho anazuiliwa nchini Paraguay kwa tuhuma za kuwa na posipoti feki. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2002 alifika Paraguay, Jumatano, Machi 4 kwa ajili ya hafla ya kujitolea lakini alikamatwa na maafisa wa polisi katika hoteli yake. Kulingana na ripoti za La Nacion, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 na kaka yake Roberto walikuwa na pasipoti zenye majina yao lakini uraia wa Paraguay. Waziri wa Usalama wa Ndani, Euclides Acevedo alisema kuwa, wawili hao walikuwa wakichunguzwa na wala hawakuwa wamekamatwa na watalazimika kujitetea. Kisha itabainishwa ikiwa watakamatwa au la. Aliongeza kuwa, Ronaldihno na kaka yake walikuwa wakishirikiana vyema na polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako