• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Michel Platini ashindwa rufaa aliyokata Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-03-06 10:36:19

    Kiongozi wa zamani wa Chama cha Soka cha Ulaya (UEFA), Michel Platini ameshindwa rufaa aliyokata Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya kupinga adhabu ya kufungiwa miaka minne kujihusisha na soka. Kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa alifungiwa baada ya kubainika kuwa alipokea malipo ya dola milioni 2 za Kimarekani kutoka kwa rais wa zamani wa Fifa, Sepp Blatter mwaka 2011. Jana, jopo la majaji saba katika mahakama hiyo inayoendesha shughuli zake jijini Strasbourg limeamua kuwa adhabu aliyopewa Platini ya kufungiwa kujihusisha na shughuli zinazohusiana na mpira wa miguu, ni halali. Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu, Fifa, lilimfungia Platini, likimvua umakamu wa rais, mwaka 2015 kutokana na malipo aliyopokea kutoka kwa Blatter, hukumu iliyosababisha mashambulizi makali ya kujibu mapigo kutoka kwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 64 na pia kuvurugika kwa mahusiano na mshirika wake wa zamani, Blatter.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako