Endapo atashinda pambano la tarehe 21 mwezi huu nchini Ujerumani, bondia Hassan Mwakinyo wa Tanzania ataandika historia mpya. Mwakinyo ana historia katika ndondi baada ya ile aliyoiweka mwaka 2018 nchini Uingereza alipomchapa Samm Eggington kwa TKO katika raundi ya pili katika pambano la raundi 10. Machi 21, Mwakinyo, ambaye ni bondia namba moja nchini Tanzania uzani wa Super Welter, atapambana na bondia Jack Culcay katika mji wa Bayerhalle, Wuppertal, kule Ujerumani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |