• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kombe La Mapinduzi Kuboreshwa Ili Liwe Na Sura Ya Muungano.

    (GMT+08:00) 2020-03-06 18:42:26

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekubaliana kuboresha kombe la Mapinduzi ili liwe na sura ya Muungano kwa kuhakikisha mfumo wa uendeshaji wa kombe hilo unafuata taratibu za muungano pamoja na kutumia wachezaji wenye sifa ambazo zinatumika katika ligi nyingine. Makubaliano hayo yamefikiwa jumatano visiwani Zanzibar katika katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika tarehe 02 Julai 2019 jijini Dodoma kilichokua na lengo la kubainisha maeneo ya ushirikiano pamoja na kujadili mapendekezo ya maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Wizara zenye dhamana ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo SMT na SMZ.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako