• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yazitaka serikali za nchi zote kutilia maanani maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-06 19:09:33

    Shirika la Afya la Duniani (WHO) limetoa onyo kwa serikali za nchi zote duniani kuwa virusi vya korona (COVID-19) sio mazoezi, bali ni jambo linatokiwa kupewa umuhimu mkubwa.

    Mkurugenzi mkuu wa WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema, maambukizi ya COVID-19 yanaweza kuzuiliwa endapo hatua, uratibu na mtazamo wa pamoja wa pande zote unaojumuisha taasisi zote za serikali utachukuliwa.

    Wakati huohuo, kiongozi wa tume ya pamoja ya China na WHO inayoshughulikia COVID-19 Bw. Bruce Aylward amesifu jitihada za China katika kupambana na ugonjwa huo. Akinukuliwa na gazeti la New York Times, Aylward amesema bado inawezekana kudhibiti maambukizi hayo kama nchi zitachukua hatua za haraka, kwa kuwa bado halijatokea janga la kimataifa.

    Aylward ambaye alitembelea China kwa muda wa wiki mbili mwanzoni mwa Februari, amepuuza tuhuma kuwa kesi za COVID-19 nchini China hazijapungua. Amesema alipokuwa China idadi ya watu waliosubiri kupimwa virusi hivyo ilifikia kilele cha elfu 46 kwa siku, na alipoondoka China, idadi hiyo ilishuka na kufikia 13,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako