Chama hicho kina wanachama 14.
Wanzilishi wa chama hicho wanasema kuwa wana biashara karibu 300 ikiwa ni pamoja na mashirika ya ushauri kutoka Ulaya, yanayofanya kazi nchini humo.
Mmoja wa wafanyabiashara wa kigeni ambaye amekuwa akisisitiza uundaji wa chama hicho,Giovanni Davite, amesema walianza wazo la kuwa na chama hicho kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache wa Ujerumani ambao walitaka kujenga uhusiano na kukuza biashara Rwanda.
Balozi wa Tume ya Umoja wa Ulaya nchini Rwanda Nicola Bellomo, ambaye aliongoza uzinduzi wa chama hicho amesema kitachochea maamuzi kama mazungumzo ya hivi karibuni kuhusu udhibiti wa tasnia ya chakula na dawa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |