• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei ya nyanya yapungua

    (GMT+08:00) 2020-03-06 20:09:00

    Bei ya nyanya ambayo imekuwa imepanda nchini Kenya sasa imeanza kushuka.

    Katika kipindi cha chini ya wiki tatu, bei ya bidhaa hiyo imeshuka kwa zaidi ya asilimia 50 kulingana na Mwenyekiti wa Kundi la Wauzaji Nyanya katika mji wa magharibi mwa Kenya wa Kisumu BwTom Justo.

    Kwa sasa, alisema wauzaji bidhaa wanauza nyanya kwa bei ya jumla ya Sh6,000 kutoka kwa Sh15,000 kwa kreti moja katikati mwa mwezi uliopita.

    Alieleza kwamba bei ya zao hilo huenda ikashuka zaidi hadi kati ya Sh3,000 na Sh4,000 katika kipindi cha mwezi mmoja ujao huku vua kubwa zikitarajiwa kupungua.

    Bw Justo alisema bado kuna upungufu wa bidhaa hiyo Kenya ambapo kiwango kilichopo hakiwezi kutosheleza wateja, hivyo kufanya wafanyabiashara kuagizia bidhaa hiyo kutoka kwa wakulima wa Uganda.

    Mfanyabiashara huyo alifafanua kwamba zao hilo nchini Kenya liliathiriwa pakubwa na ugonjwa ambao ni hatari zaidi miongoni mwa maradhi yote ya nyanya.

    Ugonjwa huo husababishwa na wadudu wanaoenea katika mmea wa nyanya hasa wakati wa msimu wa unyevunyevu na husambaa kwa kasi huku ukisababisha matawi kukauka, kuoza na kuanguka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako