Hata hivyo, ripoti hiyo imeonyesha kuwa upande wa uchukuzi wa mizigo uliimarika huku idadi ya watu wanaosafiri kupitia treni ikipungua kwa watu 200, 000.
Idadi ya abiria wanaotumia SGR ilipungua kutoka milioni 1.38 kwa kipindi kama hicho mwaka wa 2018 hadi 1.18 milioni mwaka jana.
Hii inaashiria kuwa sheria kali zilizowekwa katika saa za kuabiri treni na ushindani kutoka kwa kampuni za mabasi na ndege zinazolipisha bei nafuu zimewafanya abiria wengi kuacha kutumia SGR.
Kulingana na KNBS mapato ya shilingi bilioni 4.09 ya biashara ya kubeba mizigo na SGR kwa miezi hiyo tisa ya mwaka jana, ilikuwa mara mbili ya mwaka wa 2018.
Wafanyabiashara walianza kulipa Sh51, 275 kwa kasha la futi 20 na Sh70,000 kwa kasha la futi 40 ambayo ni mara mbili ya bei ya mvuto ya Sh25,000 hadi Sh35,000.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |