• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 300 wathibitishwa kuambukizwa virusi vipya vya Corona nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2020-03-07 18:27:12

    Hadi kufikia jana idadi watu walioambukizwa virusi vipya vya Corona (COVID-19) nchini Marekani imeongezeka na kufikia 330, na kati yao 14 wamefariki dunia.

    Jana pia makamu wa Rais wa Marekani Bw. Mike Pence alisema watu 21 waliokuwa kwenye Meli ya kitalii ya Grand Princes wamegunduliwa kuwa na virusi hivyo, ikiwa ni pamoja na wahudumu 19 na abiria wawili. Meli hiyo imeripotiwa kuwa na jumla ya watu 3000, lakini ni watu 46 ndio waliopimwa, watu 24 wamethibitishwa kuwa hawajaambukizwa na mwingine mmoja hali yake bado haijulikani.

    Meli ya Grand Princes inamilikiwa na kampuni moja inayomiliki meli ya Diamond Princes ambayo watalii 700 waliokuwa kwenye meli hiyo, walithibitishwa kuambukizwa virusi vipya vya Corona baada ya upimaji nchini Japan.

    Bw. Pence amesema kila abiria kwenye meli hiyo atapimwa, na meli hiyo itaelekezwa kwenye bandari isiyo ya kibiashara na abiria watakaothibishwa kuambukizwa watawekwa kwenye karantini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako