• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaeneza elimu za COVID-19 kwa simu za mkononi

    (GMT+08:00) 2020-03-08 17:42:23

    Matumizi ya simu za mkononi ya watu wengi nchini Kenya yanageuka kuwa mbinu ya nchi hiyo kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19).

    Japo hadi sasa Kenya haijarekodi kesi yoyote ya maambukizi ya ugonjwa huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeainisha Kenya kama nchi ya sita yenye hatari barani Afrika.

    Waziri wa Afya ya Kenya Mutahi Kagwe Ijumaa alitangaza hatua kadhaa za kuzuia virusi nje ya mipaka yake, ambazo ni pamoja na kuchunguza abiria wanaoingia nchini humo kwa njia yoyote, kufuta mikutano yote ya kimataifa, kuanzisha vitengo maalum vinavyoshughulikia watu wanaohisiwa na kuongeza mwamko wa raia. Amesema nchi hiyo imezindua huduma ya bure ya SMS kutuma habari kwa simu za mkononi, ili kila mkenya apate habari juu ya ugonjwa huo, na nini cha kufanya ili kuepusha maambukizi ya virusi.

    Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano ya Habari ya Kenya zinaonesha kuwa, kuna zaidi ya watumiaji milioni 53 wa simu za mkononi nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako