• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yakanusha taarifa ya Ethiopia juu ya azimio la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu bwawa la GERD

    (GMT+08:00) 2020-03-08 17:48:06

    Misri jana ilikanusha taarifa iliyotolewa juzi Ijumaa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia juu ya azimio lililopitishwa na Baraza la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Machi 4 kuhusu bwawa la GERD.

    Kwenye taarifa yake, Wizara ya Mambo ya nje ya Misri amesema taarifa ya Ethiopia "haifai, si ya kidiplomasia, na inaleta fedheha kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na nchi wanachama wake"

    Serikali ya Ethiopia Ijumaa ilikataa azimio jipya lililopitishwa na Jumuiya hiyo juu ya machafuko ya bwawa la GERD, ikisisitiza kuwa azimio hilo linaunga mkono nchi moja mwanachama bila ya kuzingatia ukweli muhimu wa kiini cha mazungumzo ya GERD. Jumatano mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu walieleza kukataa kudhuru haki za kihistoria za Misri katika maji ya mto Nile kwa kujenga bwawa la GERD.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako