• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa msaada wa dola za kimarekani milioni 20 kuiunga mkono WHO kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-08 17:58:51

    Serikali ya China imeamua kutoa msaada wa dola za kimarekani milioni 20 kwa Shirika la Afya Duniani WHO ili kuliunga mkono kuanzisha ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19.

    Hivi sasa maambukizi hayo yamesambaa kwenye sehemu mbalimbali duniani, na inahitajika sana kuanzisha ushirikiano wa kimataifa wa kukinga na kudhibiti ugonjwa huo. Hatua ya China kutoa fedha ni kujibu wito wa WHO na kuliunga mkono kwa vitendo halisi shirika hilo kufanya kazi maalumu katika shughuli za kupambana na virusi hivyo, hasa kuzisaidia nchi zilizokuwa na mfumo dhaifu wa afya ya jamii kujilinda na kukabiliana na maambukizi hayo.

    Virusi havijali mipaka, kusaidia mtu mwengine ni sawa na kujisaidia mwenyewe. China itaendelea kushirikiana na nchi mbalimbali na kutoa mchango katika kulinda usalama wa afya ya kikanda na kimataifa, na kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako