• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya nchi na sehemu zinazoathiriwa na COVID-19 duniani yazidi 100

    (GMT+08:00) 2020-03-09 09:18:43

    Shirika la afya duniani WHO limesema, kutokana na ripoti kutoka nchi mbalimbali, idadi ya nchi na sehemu zilizoathiriwa na nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vipya ya korona imefikia 101.

    Ripoti kutoka shirika hilo imeonesha kuwa idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa nje ya China imeongezeka kwa watu 3,610 kuliko siku iliyopita na kufikia 24,727, na idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo imeongezeka kwa watu 71 na kufikia 484.

    Takwimu zimeonesha kuwa, hadi kufikia tarehe 8, idadi ya jumla ya wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa COVID-19 iliongezeka kwa watu 3,656 kuliko siku iliyopita, na kufikia 105,586, na idadi ya vifo imeongezeka kwa 98 na kufikia 3,584.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako